Mwanamke anayekhofia kupata hedhi katika hajj kuweka sharti

Swali: Je, mwanamke anayekhofia kupata hedhi anaruhusiwa kuweka sharti wakati wa kuhirimia?

Jibu: Sifahamu kizuizi chochote. Lakini katika hajj hapana, kwa sababu anatakiwa kusubiri, kwani katika hijjah ni lazima mtu afanye Twawaaf. Hali ya hedhi ni suala linatakiwa kuzingatia… lakini ni jambo haliko mbali, kwa sababu inaweza kumsumbua kwa muda mrefu. Inaweza kusemwa pia kuwa hata katika hijjah ikiwa mwanamke amefika mapema au kuchelewa kidogo, anaweza kuwa safi kabla ya shughuli za ibada, lakini ikiwa atafika akiwa amechelewa sana na anaogopa kucheleweshwa au kukosa mambo kadhaa, basi ikiwa kuna haja ya kuweka sharti, hakuna tatizo. Kimsingi jambo hili linakubalika. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia Dhwuba’aah ambaye alikuwa mgonjwa:

“Fanya hijjah na uweke sharti.”

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24964/هل-تشترط-المراة-عند-احرامها-ان-خافت-العادة
  • Imechapishwa: 14/01/2025