41 – Ahmad bin Humayd ametuhadithia: Abu Bakr ametuhadithia, kutoka kwa Abu Haswiyn, kutoka kwa Abu Swaalih, kutoka kwa Abu Hurayrah, ambaye ameeleza:

”Bwana mmoja alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kusema: ”Ee Mtume wa Allaah, niusie, na ufupishe ili niweze kufahamu.” Akasema: ”Usikasirike.” Akamuuliza mara moja au mara mbili, na kila mara anamwambia: ”Usikasirike.”

42 – Musaddad ametuhadithia: Abul-Ahwasw ametuhadithia, kutoka kwa Sa´iyd bin Masruuq, kutoka kwa Abu Haazim, kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh), ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Si mwenye nguvu yule mwenye kuwashinda watu; lakini mwenye nguvu kikweli ni yule mwenye kuishinda nafsi yake.”

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Ismaa´iyl al-Bukhaariy (a.f.k 256)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Birr-ul-Waalidayn, uk. 138-139
  • Imechapishwa: 14/01/2025