22. Unapoingia msikitini wakati imamu anatoa Khutbah

39 – Abu Nu´aym ametuhadithia: Sufyaan ametuhadithia, kutoka kwa Abu Hayyaan at-Taymiy, kutoka kwa Ibraahiym at-Taymiy, aliyesema:

”Sijapato kuyalinganisha maneno yangu na matendo yangu, isipokuwa nilichelea nisije kuwa mwenye kukadhibisha.”

40 – Aadam ametuhadithia: Shu´bah ametuhadithia, kutoka kwa ´Amr bin Diynaar, kutoka kwa Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh), ambaye amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Anapokuja mmoja wenu na huku imamu anakhutubu, basi aswali Rak´ah mbili.”

Hayo ndio ambayo nami nasema:

Sufyaan bin ´Uyaynah amesema:

”Yule asiyejua na akajua kuwa yeye hajui, basi huyo kwa hakika ndiye mwanachuoni.”

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Ismaa´iyl al-Bukhaariy (a.f.k 256)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Birr-ul-Waalidayn, uk. 136-137
  • Imechapishwa: 14/01/2025