37 – ´Aliy bin ´Abdillaah ametuhadithia: Sufyaan ametuhadithia: Ibraahiym at-Taymiy (Rahimahu Allaah) amesema:
”Nilijiwazia niko Peponi ambapo nikila katika vyakula vyake, nikinywa katika vinywaji vyake, nikiishi na wakazi wake na nikipata yale ninayotamani. Kisha nikasema: ”Ee nafsi yangu, tamani kitu!” Ikasema: ”Natamani nirudi ulimwenguni ili nizidishe matendo na hivyo kuzidishiwa thawabu.” Kisha nikajiwazia niko Motoni ambapo nikila katika chakula chake kibaya, nikinywa maji yake ya moto na nikiishi na wakazi wake. Kisha nikasema: ”Ee nafsi yangu, tamani kitu!” Ikasema: ”Natamani nikirudi ulimwenguni nitubie ili nisalimike kutokamana na yale niliyomo.” Ndipo nikaiambia: ”Ee nafsi yangu, uko katika kile unachotamani. Hivyo basi hakikisha unafanya matendo!”
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Ismaa´iyl al-Bukhaariy (a.f.k 256)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Birr-ul-Waalidayn, uk. 134-135
- Imechapishwa: 14/01/2025
37 – ´Aliy bin ´Abdillaah ametuhadithia: Sufyaan ametuhadithia: Ibraahiym at-Taymiy (Rahimahu Allaah) amesema:
”Nilijiwazia niko Peponi ambapo nikila katika vyakula vyake, nikinywa katika vinywaji vyake, nikiishi na wakazi wake na nikipata yale ninayotamani. Kisha nikasema: ”Ee nafsi yangu, tamani kitu!” Ikasema: ”Natamani nirudi ulimwenguni ili nizidishe matendo na hivyo kuzidishiwa thawabu.” Kisha nikajiwazia niko Motoni ambapo nikila katika chakula chake kibaya, nikinywa maji yake ya moto na nikiishi na wakazi wake. Kisha nikasema: ”Ee nafsi yangu, tamani kitu!” Ikasema: ”Natamani nikirudi ulimwenguni nitubie ili nisalimike kutokamana na yale niliyomo.” Ndipo nikaiambia: ”Ee nafsi yangu, uko katika kile unachotamani. Hivyo basi hakikisha unafanya matendo!”
Muhusika: Imaam Muhammad bin Ismaa´iyl al-Bukhaariy (a.f.k 256)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Birr-ul-Waalidayn, uk. 134-135
Imechapishwa: 14/01/2025
https://firqatunnajia.com/21-tamani-kitu/