Amefanya Sa´y kabla ya Twawaaf

Swali: Nini ninachomlazimu yule aliyefanya Sa´y kabla ya Twawaaf kutokana na ujinga wake, akapunguza nywele zake na akafanya yale anayofanya aliyetoka katika Ihraam ilihali bado yuko Makkah? Aidha kipi kinachomlazimu akishatoka Makkah?

Jibu: Hakuna tatizo kwake. Hapana neno kwake ikiwa amefanya Sa´y kabla ya Twawaaf. Lakini Sunnah ni yeye afanye Twawaaf kwanza ndio ndio alete Sa´y. Isitoshe imethibiti kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba mtu mmoja alimuuliza:

“Ee Mtume wa Allaah, nimefanya Sa´y kabla ya kutufu?” Akasema: “Hapana vibaya.”

Sunnah ni kwamba atufu kwanza ndio afanye Sa´y. Kwa hivyo ikiwa mtu atafanya Sa´y kwa ujinga au kwa kusahau, kisha akatufu na halafu akapunguza nywele zake, jambo hilo limekamilika.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25143/ما-حكم-من-سعى-قبل-الطواف-جهلا
  • Imechapishwa: 07/02/2025