Ayaendee maji 10 km au afanye Tayammum?

Swali: Nikiwa maji ambapo maji yamekatika inafaa kwangu kufanya Tayammum au ni lazima kwenda kwa gari yangu maeneo ambapo yanapatikana maji ambapo ni umbali wa takriban 10 km?

Jibu: Maadamu kuna maji, basi ajitahidi kuyafikia. Kidesturi maji hayo yanazingatiwa kuwa karibu. Basi ni lazima kutawadha na asifanye Tayammum. Lakini yakiwa mbali, kwa namna ya kwamba yanamchukulia muda wake mwingi au wakati wa swalah ukampita, katika mazingira hayo ni sawa akafanya Tayammum.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25142/هل-يجب-البحث-على-من-فقد-الماء-قبل-التيمم
  • Imechapishwa: 07/02/2025