Amechoka sana na anashindwa kusubiria swalah

Swali: Kuna msichana amechelewesha Maghrib kwa sababu ya usingizi na hakuiswali isipokuwa asubuhi. Ni ipi hukumu?

Jibu: Haijuzu kuchukulia wepesi swalah mpaka ukatoka wakati wake. Ikiwa mtu amelala basi anatakiwa kuhakikisha kuna wa kumwamsha. Haiwezekani kuchelewesha Maghrib na ´Ishaa mpaka wakati wa Fajr. Bali ni wajibu kuiswali swalah ndani ya wakati wake. Ni lazima kwa msichana huyu kuwaomba wanafamilia yake kumwamsha.

Ikiwa tutakisia kuwa kuna dharurah na akachelea kuwa asipochanganya Maghrib na ´Ishaa basi usingizi utamshinda nguvu na asiweze kuamka isipokuwa wakati wa Fajr, basi hapana vibaya katika hali hiyo akakusanya ´Ishaa na Maghrib ili asikose ´Ishaa ndani ya wakati wake. Jambo hilo haliwi isipokuwa wakati wa dharurah kama kwa mfano msichana huyo amekosa usingizi nyusiku kadhaa, mgonjwa au mfano wake.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/27-28)
  • Imechapishwa: 11/05/2026