22 – Pengine ukaona kuwa haya yanapingana na yale yaliyosemwa na Shaykh Qaasim katika “Sharh Ahaadiyth-il-Ikhtiyaar” wakati aliponukuu kutoka kwa Ibn Abiy Shaybah, ambaye amesema: Wakiy´ amesimulia kutoka kwa Muusa bin ´Umayr, kutoka kwa ´Alqamah bin Waa-il bin Hujr, kutoka kwa baba yake, aliyesema:
”Nilimuona Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiweka mkono wake wa kulia juu ya mkono wake wa kushoto ndani ya swalah chini ya kitovu.”[1]
Halafu akasema kwamba ”cheni ya wapokezi ni nzuri”.
Kuhusu kuthibiti kwa ziada ya “chini ya kitovu” ni jambo la kuangalia vyema, bali hilo ni kosa. Chanzo chake ni kusahau, kwani nimepitia nakala sahihi ya al-Muswannaf na nikaona ndani yake Hadiyth hii kwa cheni hii ya wapokezi na kwa matamshi haya, isipokuwa ndani yake hakuna “chini ya kitovu”. BAada ya Hadiyth hii akataja masimulizi ya an-Nakha´iy, na tamko lake liko karibu na tamko la Hadiyth hii, na mwishoni mwake kuna sentesi “ndani ya swalah chini ya kitovu.” Huenda macho ya mwandishi yaliteleza kutoka sehemu moja kwenda nyingine ambapo akajumuisha maneno ya mwanafunzi wa Maswahabah ndani ya maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kinachothibitisha niliyosema ni kwamba nakala zote hazikukubaliana juu ya ziada hii, na kwamba wanazuoni wengi wa Hadiyth, ambao wamepokea Hadiyth hii, hawakutaja sentesi inayosema “chini ya kitovu”. Bali sijawahi kuona wala kusikia yeyote miongoni mwa wanazuoni aliyetaja Hadiyth hii kwa ziada ya ”chini ya kitovu” isipokuwa al-Qaasim.
23 – Ibn ´Abdil Barr, hafidhi wa zama zake, amesema katika ”at-Tamhiyd”:
”ath-Thawriy na Abu Haniyfah wamesema kuwa mikono inatakiwa kuwekwa chini ya kitovu. Imepokelewa hivyo kutoka kwa ´Aliy na Ibraahiym an-Nakha´iy, lakini haikuthibiti kutoka kwao.”[2]
Lau Hadiyth hii kwa tamko hili katika ”al-Muswannaf” ya Ibn Abiy Shaybah ingelikuwa ni Swahiyh, basi angeitaja, kwa sababu amenukuu sana katika mlango huu na mingineyo kutoka kwa Ibn Abiy Shaybah.
24 – Ibn Hajar, hafidhi wa zama zake, amesema katika ”Fath-ul-Baariy”:
”Ibn Khuzaymah amepokea Hadiyth ya Waa-il kwamba (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliweka mikono yake juu ya kifua chake. al-Bazzaar amepokea “karibu na kifua chake”. Ahmad amepokea mfano wake kutoka kwa Hulb.”[3]
Amesema katika kitabu “ad-Diraayah fiy Takhriyj Ahaadiyth-il-Hidaayah”:
”Cheni ya wapokezi ya masimulizi ya ´Aliy ni dhaifu. Isitoshe inapingana na Hadiyth ya Waa-il bin Hujr inayosema:
”Niliswali pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam); akauweka mkono wake wa kulia juu ya mkono wake wa kushoto juu ya kifua chake.”
Akaashiria hilo katika ukaguzi wa Hadiyth ya ar-Raafi´iy[4]. Kama ziada ingelikuwa katika ”al-Muswannaf”, basi angeitaja, kwa sababu vitabu vyake vimejaa Hadiyth na masimulizi yake, kama alivosema as-Suyuutwiy katika “Sharh-ul-Alfiyyah”.
25 – Yaliyo dhahiri ni kwamba az-Zayla´iy, licha ya kwamba alijitahidi sana kukusanya dalili za madhehebu hakupata ziada hiyo. Lau angeipata basi angeitaja. Isitoshe alikuwa ni miongoni mwa watu wenye upeo mkubwa zaidi wa maarifa.
[1] al-Muswannaf (1/390).
[2] at-Tamhiyd (2/75).
[3] Fath-ul-Baariy (2/224).
[4] at-Talkhiysw al-Habiyr (1/224).
- Muhusika: ´Allaamah Muhammad Hayaah as-Sindiy (afk. 1163)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fath-ul-Ghafuur fiy Wadhw´-il-Aydiy ´alaas-Suduur, uk. 49-57
- Imechapishwa: 11/05/2026

Muhusika: ´Allaamah Muhammad Hayaah as-Sindiy (afk. 1163)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fath-ul-Ghafuur fiy Wadhw´-il-Aydiy ´alaas-Suduur, uk. 49-57
Imechapishwa: 11/05/2026
https://firqatunnajia.com/05-hakuna-kilichothibiti-kuhusu-kuweka-mikono-chini-ya-kitovu/