18 – Mulaa Daad al-Hindiy amesema katika “Sharh-ul-Hidaayah”:
”Ikiwa Hadiyth ya kuweka mikono chini ya kitovu ni dhaifu na inapingana na tafsiri ya ´Aliy kwamba alitafsiri maneno Yake Allaah (Ta´ala):
فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ
”Basi swali na uchinje kwa ajili ya Mola wako!”
kwamba ni kuweka mikono juu ya kifua, basi ni lazima kufanyiwa kazi Hadiyth ya Abu Waa-il iliyotajwa na an-Nawawiy.”
19 – at-Twabaraaniy amesema: Bishr bin Muusa ametuhadithia: Muhammad bin Hujr bin ´Abdil-Jabbaar bin Waa-il bin Hujr al-Hadhwramiy ametukhabarisha: Ami yangu Sa´iyd bin ´Abdil-Jabbaar ametuhadithia, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa mama yake Umm Yahyaa, kutoka kwa Waa-il, ambaye amesema:
”Nilihudhuria swalah pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)… Kisha akainua mikono yake wakati wa Takbiyr mpaka ilipolingana na masikio yake. Kisha akaweka mkono wake wa kulia juu ya mkono wake wa kushoto juu ya kifua chake.”
al-Bazzaar amesimulia mfano wake kutoka kwake. Vivyo hivyo ndivo amefanya al-Bayhaqiy katika ”as-Sunan” yake. Katika cheni zote za wapokezi yumo Muhammad bin Hujr. al-Bukhaariy amesema kwamba ”kuna uchunguzi fulani juu yake”[1]. Wengine wamesema kuwa anazo ana riwaya zisizokubalika.
20 – al-Bayhaqiy amesema: Mu-ammil bin Ismaa´iyl ameisimulia kutoka kwa ath-Thawriy, kutoka kwa ´Aaswim bin Kulayb, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Waa-il, ambaye ameeleza:
”Alimuona Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiweka mkono wake wa kulia juu ya mkono wake wa kushoto, kisha akaweka mikono hiyo juu ya kifua chake.”
Mu-ammil alikuwa mwenye kuaminika na alikuwa na kumbukumbu mbovu, kama ilivyo katika ”at-Taqriyb”[2]. Haya yanatilia nguvu yale yaliyotajwa na wanazuoni wengi kwamba Ibn Khuzaymah ameipokea Hadity hii katika ”as-Swahiyh” yake[3].
21 – an-Nawawiy amesema katika “Khulaaswat-ul-Ahkaam” kwamba Waa-il amesema:
”Niliswali pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Akauweka mkono wake wa kulia juu ya mkono wake wa kushoto.”
[1] at-Taariykh al-Kabiyr (1/69).
[2] Taqriyb-ut-Tahdhiyb, uk. 555.
[3] as-Swahiyh (1/242-243).
- Muhusika: ´Allaamah Muhammad Hayaah as-Sindiy (afk. 1163)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fath-ul-Ghafuur fiy Wadhw´-il-Aydiy ´alaas-Suduur, uk. 40-49
- Imechapishwa: 11/05/2026

Muhusika: ´Allaamah Muhammad Hayaah as-Sindiy (afk. 1163)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fath-ul-Ghafuur fiy Wadhw´-il-Aydiy ´alaas-Suduur, uk. 40-49
Imechapishwa: 11/05/2026
https://firqatunnajia.com/04-alimuona-mtume-akiswali-kwa-kuweka-mikono-juu-ya-kifua/