03. Weka mkono wako wa kulia juu ya mkono wako wa kushoto juu ya kifua

14 – Abush-Shaykh na al-Bayhaqiy wamesimulia kutoka kwa Anas, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), na Ibn Abiy Haatim, Ibn Shaahiyn katika “as-Sunan”, Ibn Marduuyah na al-Bayhaqiy wamesimulia kutoka kwa Ibn ´Abbaas, ambaye amesema kuhusiana na maneno Yake (Ta´ala):

فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ

”Basi swali na uchinje kwa ajili ya Mola wako!”

”Ni kuweka mkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto katika kifua ndani ya swalah.”

15 – al-Khaazin amesema:

”Ibn ´Abbaas amesema kuhusiana na maneno Yake (Ta´ala):

فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ

”Basi swali na uchinje kwa ajili ya Mola wako!”

”Maana yake ni kwamba weka mkono wako wa kulia juu ya mkono wa kushoto katika kifua.”

16 – Amesema katika “Mi´raaj-ud-Diraayah Sharh-ul-Hidaayah”:

”Wakati ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) aliposoma Aayah hii, aliweka mkono wake wa kulia juu ya mkono wake wa kushoto juu ya kifua chake.”

17 – Baadhi yao wamenakili kwamba al-Haakim amesema:

”Hii ndiyo tafsiri nzuri zaidi ya Aayah hii.”

Wako wanaosema kwamba ikiwa Aayah kweli inakusudia hivo, basi maana yake ni weka mikono karibu na kifua, kwa maana nyingine chini ya kifua. Tafsiri hiyo ni kosa kiakili na kinukuu, basi zingatia hilo.

  • Muhusika: ´Allaamah Muhammad Hayaah as-Sindiy (afk. 1163)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fath-ul-Ghafuur fiy Wadhw´-il-Aydiy ´alaas-Suduur, uk. 38-40
  • Imechapishwa: 11/05/2026