Swali: Ni ipi hukumu ya kuwachukua picha wanawake kwa ajili ya kumbukumbu?

Jibu: Ni haramu na haijuzu kuwachukua picha wanawake na wasiokuwa wanawake kwa ajili ya kumbukumbu. Kwa sababu kunatokana na malengo haramu. Kile ambacho lengo lake ni haramu basi njia inakuwa na hukumu hiyohiyo. Ni haramu kuhifadhi picha kwa sababu Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema kuwa Malaika hawaingii ndani ya nyumba ilio na picha. Hata hivyo kikosi kikubwa cha wanazuoni wamesema kuwa ikiwa picha ni zenye kutwezwa, kama mfano picha zinazokuwa kwenye magodoro au mito – hazina neno. Licha ya kwamba tahadhari na salama zaidi ni mtu asizihifadhi ingawa ni katika hali ya kuzitweza.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/351)
  • Imechapishwa: 11/05/2026