Ameapa kufunga kwa mwezi mara moja akipona

Swali: Mama yangu alipatwa na maradhi yaliyompelekea kulazwa. Hayo yalitokea takriban miaka mitatu nyuma. Wakati wa maradhi yake ameapa kwamba atafunga kila mwezi siku moja ambapo mpaka hii leo anaendelea kufunga siku moja kwa kila mwezi. Mama yangu anauliza kama kuna kafara nyingine badala ya funga aliyojilazimisha nafsi yake? Yote hayo ni kwa sababu anaogopa baadhi ya siku asije kusahau kufunga au akapatwa na maradhi yatayomzuia kufunga au kitu kingine.

Jibu: Hiki ni kitu kidogo na chepesi kwa yeye kufunga siku moja kwa kila mwezi. Anaweza kufanya siku hiyo ikawa jumatatu au alkhamisi. Hakuna ubaya juu ya hilo. Midhali ameapa hali ya kuilazimisha nafsi yake jambo hilo basi hii ni nadhiri iliofungika kwa kiapo. Hivyo ni lazima kwake kutimiza kile alichowekea nadhiri kwa ajili ya Allaah (´Azza wa Jall). Ni kitu ambacho hakimdhuru. Tukikadiria kuwa ameacha kufanya hivo kwa kusahau – midhali ni mwenye kutilia umuhimu jambo hilo – tunatarajia kwamba Allaah atamsamehe.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (06) http://binothaimeen.net/content/6691
  • Imechapishwa: 02/11/2020