Akimfanyia kila kitu mke wake

Abu ´Aliy at-Tanuukhiy amesimulia katika “an-Nashwaar” yake kutoka kwa ´Uthmaan bin Muhammad as-Sulamiy: Ibn Manju al-Qaa´id amenihadithia: Kijana wa Ibn-ul-Marzuuq amenihadithia:

“Mmiliki wangu alininunulie mjakazi na baadaye akanioza naye. Nikampenda lakini yeye akanichukia. Mpaka nikachoka na mwishowe nikamwambia: “Umeachika mara tatu ukinizungumzisha kitu mpaka na mimi nikuzungumzishe kitu hicho. Ni mangapi nakufanyia?” Papo hapo akasema: “Umeachika mara tatu (أنتَ طالق).” Nikashindwa la kusema na baadaye nikaelekezwa kwa Muhammad bin Jariyr. Akanambia: “Kuwa pamoja naye baada ya uliyosema kumwambia: “Umeachika mara tatu nikikutaliki.

Shaykh wa Hanaabilah Ibn ´Aqiyl amesema:

“Lipo jibu lingine, mwanamme akasema kama alivomwambia (أنتَ طالق).” Hiyo ina maana kwamba anazungumzisha kwa dhamira ya kiume (أنتَ). Katika hali hiyo hakuvunja kiapo.”

Abul-Faraj bin al-Jawziy amesema:

“Haikuwa inamlazimu mwanamme kumwambia hayo papo hapo. Ajichelewesha mpaka wakati wa kifo.”

Akisema kwa njia ya kuuliza na akakusudia kuwa ameachika kutokamana na kifungo au kwamba ana ugumu wa kuzaa (طلق), basi talaka haitopita.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (14/278)
  • Imechapishwa: 02/11/2020