Ameacha anausia kutembelewa kila alkhamisi

Swali: Kuna ndugu yangu amefariki. Kabla ya siku chache kufa, aliacha anausia familia yake, mke na watoto wamtembelea kwenye kaburi lake kila siku ya alkhamisi. Je, wasia kama huu utekelezwe?

Jibu: Ama suala la kwenda kumtembelea, hii ni Sunnah hata kama asingewausia. Wanatakiwa kwenda kumtembelea, kumuombea na kumtolea salamu. Ama kuwekea kikomo cha siku, hili halina msingi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwekea mpaka kuyatembelea makaburi kwa siku maalum.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Fathul_25-11-1434_0.mp3
  • Imechapishwa: 20/09/2020