Swali: Kuchukua Fatwa ya mwanachuoni inachukuliwa kuwa ni kufuata kipofu (Taqliyd) na hilo linaingia katika ufuataji kipofu wenye kulaumika au wenye kusifika?

Jibu: Kwa mtu ambaye sio msomi ni sawa akamuuliza mwanachuoni na akachukua Fatwa yake. Huu ndio upeo wake. Allaah (Ta´ala) Amesema:

فَاسْأَلُواْ أَهْلَ الذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لاَ تَعْلَمُونَ

“Basi waulizeni wenye ukumbusho kama nyinyi hamjui.” (16:43)

Ama mwanachuoni haijuzu kwake kuchukua kauli ya yeyote isipokuwa mpaka baada ya kujua dalili yake kutoka katika Kitabu na Sunnah. Ikiwa haijui kuwa ina dalili na mashiko, haijuzu kwake kuchukua kauli yake ilihali anaweza kujua kauli na Fatwa yenye dalili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/blug–1430-7-27.mp3
  • Imechapishwa: 19/04/2015