Swali: Ni ipi hukumu ya kutoka nje ya msikiti baada ya adhaana?

Jibu: Imekatazwa na haijuzu. Imethibiti kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) kwamba alimuona bwana mmoja anayetoka msikiti baada ya adhaana ambapo akasema:

“Ama huyu amemuasi Abul-Qaasim (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (22)
  • Imechapishwa: 15/10/2021