Swali: Ni ipi hukumu ya kusema “Allaah Yuko pamoja nawe” wakati wa kuachana pasina kumaanisha kuwa Allaah Yuko kila mahali?

Jibu: Allaah Yuko pamoja nawe ni utangamano [Ma´iyyah] wa kimaalum wenye sampuli ya ulinzi, nusura na msaada. Allaah Yuko na viumbe Vyake wote kwa aina ya matangamano ya kijumla na Yuko na waumini kwa aina ya matangamano maalum kwa kuwanusuru, kuwasaidia na kuwaangalia. Haya ni matangamano ya kimaalum.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (09) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/qir–14340324.mp3
  • Imechapishwa: 27/06/2015