Ni muhimu kwetu kuamini kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) yuko pamoja na viumbe lakini wakati huo huo yuko juu ya ´Arshi. Hafanani na yeyote katika sifa Zake. Huwezi katu kufikiria ni namna gani Allaah anakuwa pamoja na sisi ilihali yuko [juu] mbingunu. Tunasema kuwa Allaah (´Azza wa Jalla) halinganishwi na viumbe Vyake.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/330)
- Imechapishwa: 11/05/2023