Kutawadha kwa mujibu wa Shari’ah

Sharti ya pili ya swalah ni twahara. Swalah haikubaliwi bila ya twahara. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah haikubali swalah ya mmoja wenu anapokuwa na hadathi mpaka atawadhe.”[1]

Ni lazima mtu atawadhe kwa njia iliyoamrishwa katika Shari´ah. Akiwa na hadathi ndogo; haja ndogo au kubwa, kutokwa na upepo, kusinzia na kula nyama ya ngamia, basi atawadhe.

[1] al-Bukhaariy (135).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/362)
  • Imechapishwa: 11/05/2023