Allaah (Ta´ala) hahitajii kitu

Imaam at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

“[Allaah] hahitajii kitu:

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ

“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.” (42:11)

Hahitajii kitu miongoni mwa vitu. Neno “kitu” linahusiana na viumbe vyote. Hamuhitajii kiumbe yeyote kutokana na ukamilifu wa utajiri Wake. Maneno Yake:

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ

“Hakuna chochote kinachofanana Naye… “

Hii ni Radd kwa Mumaththilah na Mushabbihah. Maneno Yake:

وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ

“Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.”

Hii ni Radd kwa Mu´attwilah ambao wanapinga majina na sifa za Allaah. Ni Aayah ilio na Radd kwa mapote mawili:

1- Mumaththilah.

2- Mushabbihah.

Mushabbihah wanamfananisha Allaah na viumbe Vyake na wanazipigia mfano sifa za Allaah na sifa za viumbe. Ni Radd vilevile kwa Mu´attwilah ambao wanakanusha majina na sifa za Allaah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/96)
  • Imechapishwa: 31/05/2020