Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

عن أبي موسى عبد الله بن قيس الأشعري رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ((إنَّ الله تعالى يَبْسُطُ يدَه بالليلِ ليتوبَ مسيءُ النَّهارِ، ويَبْسُطُ يدَه بالنَّهارِ ليتوبَ مسيءُ الليلِ، حتى تَطْلُعَ الشَّمْسُ مِنْ مَغْرِبِهَا))

16 – Abu Muusa al-Ash´ariy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika ya Allaah (Ta´ala) anaikunjua mikono Yake usiku ili amsamehe aliyekosea mchana, na anaikunjua mikono Yake mchana ili amsamehe aliyekosea usiku mpaka pale jua litapochomoza upande wa magharibi.”[1]

وعن أبي هريرة – رضي الله عنه- قال قال رسول الله صلي الله عليه وسلم: ((من تاب قبل أن تطلع الشمس من مغربها تاب الله عليه)) (رواه مسلم)

17 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kutubu kabla ya jua kuchomoza kutoka upande wa magharibi, basi Allaah atamsamehe.”[2]

Katika Hadiyth hii kuna dalili ya kuthibitisha ya kwamba Allaah (´Azza wa Jall) yuko na mkono. Hali ni hivyo. Bali (Jalla wa ´Alaa) ana mikono miwili. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَقَالَتِ الْيَهُودُ يَدُ اللّهِ مَغْلُولَةٌ غُلَّتْ أَيْدِيهِمْ وَلُعِنُواْ بِمَا قَالُواْ بَلْ يَدَاهُ مَبْسُوطَتَانِ

“Mayahudi walisema: “Mkono wa Allaah umefumba. Mikono yao ndiyo iliyofumba na wamelaaniwa kwa waliyoyasema. Bali mikono Yake imefumbuliwa.” (05:64)

Mkono huu, bali mikono miwili hii, ambayo Allaah amejithibitishia Mwenyewe ni wajibu kwetu kuiamini na kwamba imethibiti kwa Allaah. Lakini hata hivyo haijuzu kwetu kufikiria kuwa ni kama mikono yetu. Allaah (Ta´ala) anasema katika Kitabu Chake:

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖوَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ

“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote.” (42:11)

Vivyo hivyo kila sifa utayoipitia mthibitishie nayo Allaah (´Azza wa Jall), lakini fanya hivo bila ya kuifananisha na sifa za viumbe. Kwa sababu Allaah hakuna kitu mfano Wake, si katika dhati Yake wala sifa Zake.

[1] Muslim. 

[2] Muslim.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/105)
  • Imechapishwa: 06/02/2023