Allaah Anasifika Kufanya Harakati?

Swali: Kuna yeyote katika Ahl-us-Sunnah aliyemthibitishia Allaah kuwa na Sifa ya harakati?

Jibu: Enyi ndugu zangu! Kwa nini mnapekua mambo haya? Hakukuthibiti neno harakati si kwenye Qur-aan wala Sunnah. Sisi hatusemi juu ya Allaah isipokuwa yaliyothibiti kwenye Qur-aan au Sunnah. Acheni mambo haya. Kitu ambacho hakikuja katika Qur-aan na Sunnah kiacheni.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (02) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_02.mp3
  • Imechapishwa: 31/05/2015