Allaah akipokea msamaha wa Aadam (´alayhis-Salaam)

Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:

 فَتَلَقَّىٰ آدَمُ مِن رَّبِّهِ كَلِمَاتٍ فَتَابَ عَلَيْهِ ۚ إِنَّهُ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ

“Halafu Aadam akapokea maneno kutoka kwa Mola wake na akapokea tawbah yake. Kwani hakika Yeye ndiye Mwingi wa kupokea tawbah, Mwenye kurehemu.”[1]

Akalakinishiwa na kupewa ilhamu na Allaah. Maneno aliyopewa ni maneno Yake:

رَبَّنَا ظَلَمْنَا أَنْفُسَنَا

“Ee Mola wetu! Tumezidhulumu nafsi zetu.”[2]

Akatambua dhambi yake na akamuomba Allaah msamaha wake. Ndipo Allaah akamsamehe na kumrehemu.

إِنَّهُ هُوَ التَّوَّابُ

“Kwani hakika Yeye ndiye Mwingi wa kupokea tawbah… ”

Kwa yule mwenye kutubia na kurejea Kwake. Tawbah yake ni aina mbili:

1- Kwanza kuwafikishwa.

2- Pili ni kukubali tawbah pale inapokusanya sharti zake.

 الرَّحِيمُ

“… Mwenye kurehemu.”

Mwenye kuwarehemu waja Wake. Miongoni mwa huruma Yake ni kwamba amewawafikisha kutubia na hivyo akawasamehe na kupuuzilia mbali.

[1] 02:37

[2] 07:23

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Taysiyr-ul-Kariym, uk. 40
  • Imechapishwa: 22/06/2020