Swali: Siku chache za nyuma tumesibiwa na msiba kwa kufariki kwa Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas (Rahimahu Allaah). Tumesikia jinsi baadhi ya watu wanavomtilia mashaka. Unamjua vipi? Itakuwa ni vizuri ikiwa utataja kitu kifupi kuhusu Shaykh – Allaah amrehemu.

Jibu: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas (Rahimahu Allaah) ni mwanamme aliyekuwa akijulikana kwa watu wote kuwa alikuwa ni mwanachuoni, mlinganiaji katika dini ya Allaah (´Azza wa Jall) na mtoa nasaha katika vitabu vyake vyake, vijitabu vyake na akibainisha haki. Nafasi yake inajulikana. Yule mwenye kueneza mashaka juu yake basi anaeneza mashaka kuhusu Maswahabah. Kulienezwa mashaka juu ya wanachuoni wa hapo kabla. Watu hawa wapuuzwe. Watu hawa hakuna yeyote anayesalimika nao. Wanaeneza mashaka matupu hata kwa Maswahabah, maimamu na watu wa kheri. Hakuna zama wanakosekana watu hawa. Lakini himdi zote ni Zake Allaah ya kwamba hawamdhuru yeyote isipokuwa nafsi zao wenyewe bila ya wao kujua hilo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=hyLvOyPiXUo
  • Imechapishwa: 22/06/2020