Swali: Je, ni Sunnah mtu wakati mwingine kuiga matendo yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kama vile kitanda na chakula chake?

Jibu: Ni katika kunyenyekea. Hapana  shaka kwamba ni katika kujishusha na kuivunja nafsi. Ni sawa mtu akifanya baadhi ya mambo ambayo yanapingana na anasa kwa ajili ya kuivunjisha moyo na kujizoweza uchamgamfu na unyenyekevu… lakini Allaah akikufungulia jifungue, kama alivosema ´Umar:

”Allaah akikufungulieni basi jifungueni.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anapokutana na jambo ambalo Allaah amemrahishishia, kwa mfano katika ndoa yake na Zaynab aligawa nyama na chakula kingi na akawaalika watu wa kawaida.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24333/%D9%87%D9%84-%D8%A7%D9%84%D8%AA%D8%A7%D8%B3%D9%8A-%D8%A8%D8%AA%D9%88%D8%A7%D8%B6%D8%B9-%D8%A7%D9%84%D9%86%D8%A8%D9%8A-%EF%B7%BA-%D9%81%D9%8A-%D9%85%D8%B9%D9%8A%D8%B4%D8%AA%D9%87-%D8%B3%D9%86%D8%A9
  • Imechapishwa: 30/09/2024