Mahimizo ya kuomba msamaha kabla ya alfajiri

Swali: Je, kuomba msamaha punde kidogo kabla ya kuingia alfajiri ni Sunnah?

Jibu: Ndio, Allaah amewasifu waumini pale aliposema:

وَالْمُسْتَغْفِرِينَ بِالْأَسْحَارِ

“… na waombao msamaha kabla ya alfajiri.”[1]

وَبِالْأَسْحَارِ هُمْ يَسْتَغْفِرُونَ

“… na kabla ya alfajiri wakiomba msamaha.”[2]

Kuomba msamaha ni jambo limesuniwa katika kila wakati.

[1] 03:17

[2] 51:18

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24335/هل-الاستغفار-في-السحر-سنة
  • Imechapishwa: 30/09/2024