Alaumiwe mume au mke?


Swali: Mwanamke akitoka nyumbani pasi na haja na akafanyiwa maudhiko na wanaume. Je, tumlaumu mwanamke kama jinsi tunamlaumu mwanaume pia?

Jibu: Tunawaulumu wote wawili. Tunawalaumu wote wawili, mwanaume ambaye hakumuhifadhi na mwanamke ambaye amefanya vibaya katika adabu na ameenda kinyume na linalolingana na mwanamke katika kujiheshimu.

Kutoka kwa mwanamke kuna khatari, hata kama itakuwa ni kwenda msikitini. Vipi tusemeje kutoka kwake kwenda mahala pasipokuwa msikitini? Kutoka kwa mwanamke kuna khatari. Lakini wako wapi wanaofahamu! Masuala haya ni khatari sana kwa leo juu ya qadhiya ya wanawake. Wanawake wamepewa uhuru katika pande zote. Tumeingiliwa na fikira za kimagharibi na adabu za kimagharibi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mntq-0601143503.mp3
  • Imechapishwa: 10/09/2020