Mume hana haki ya kumkataza mke kutokamana na Da´wah Salafiyyah


Swali: Mama yangu hakujaaliwa kusoma na ana ujinga. Anapenda kusikia kanda za kurekodiwa. Lakini hata hivyo baba yangu ametuwekea uzito na kutukatalia kuiingiza nyumbani. Mama yangu anauliza kama kuna neno kuiingiza bila ya yeye kujua na kusikiliza anayoweza kufaidika nayo katika mambo ya dini yake? Kwa sababu kama alivyosema hajui kusoma wala kuandika. Lau ningejua kusoma ningetosheka na hilo.

Jibu: Mke wala familia haina haki ya kukataza kuingiza kanda zenye faida. Kinachotakiwa kwake ni yeye kumshukuru Allaah juu ya neema hii kwa Allaah kuzifungua nyoyo za wanafamilia kusikiliza kanda kama hizi zenye faida.

Tukikadiria kuwa anazuia kuingiza kanda hizi, ni sawa kwa wanafamilia wakaiingiza kwa kumficha. Kwa sababu hana yeyote haki ya kumzuia yeyote kusikiliza Ukumbusho. Ikiwa mume huyu ambaye amemkatalia mke wake kuingiza au kusikiliza kanda hizi ana mashaka [juu ya kanda hizo], basi aisikilize kwanza na halafu akataze yale yasiyokuwa ya sawa. Kuhusu yale ya sawa hana haki ya kumkataza mke wake kusikiliza Ukumbusho. Wanaweza kuiingiza kwa kumficha na wakafaidika.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (01)
  • Imechapishwa: 10/09/2020