Amehisi kutokwa na damu lakini imetoka baada ya jua kuzama

Swali: Mimi ni mwanamke nilifunga siku sita za Shawwaal ambapo siku ya mwisho ya swawm nikahisi kutokwa na manjanonjano/rangi ya zambarau na damu haikutoka isipokuwa usiku. Je, swawm hii ni sahihi au nirudi kufunga tena siku hii?

Jibu: Swawm ya siku hii ni sahihi. Kwa sababu damu haikutoka isipokuwa baada ya jua kuzama. Mwanamke akihisi hedhi na isitoki isipokuwa baada ya kuzama jua, swawm yake ni sahihi. Ni mamoja iwe ya faradhi au ya Sunnah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (01)
  • Imechapishwa: 10/09/2020