al-Waswaabiy kuhusu ´Aqiydah ya Shu´ayb al-Arnaa´uut na ukaguzi wake wa Hadiyth

Swali: Ni vipi hali ya Shu´ayb al-Arnaa´uut na mtu anaweza kuchukua hukumu yake juu ya Hadiyth pindi anapohukumu kuwa ni Swahiyh au dhaifu?

Jibu: Kwa jumla uhakiki wake ni mzuri. Wakati anapohukumu Hadiyth kuwa ni Swahiyh au dhaifu, chukua kauli yake ikiwa hukukinaika kuwa amekosea. Katika hali hii utafuata kauli sahihi. Lakini endapo hukupata kauli nyingine isipokuwa ya kwake, haina neno ukaichukua.

Aliulizwa Shaykh wetu Muqbil (Rahimahu Allaah) juu yake na akafutu kama jinsi nilivyosema, kwamba mtu achukue faida kutoka katika uhakiki wake na kwamba kwa jumla unaonekana ni mzuri. Isipokuwa katika masuala ya ´Aqiydah. Ni mwenye kujeruhiwa katika masuala ya ´Aqiydah. Ama kuhusiana na uhakika wake, Takhriyj na hukumu juu ya Hadiyth, mtu anaweza kuchukua. Tunamuomba Allaah Atuongoze sisi, yeye na Waislamu wote.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://olamayemen.al3ilm.com/?ID=2402
  • Imechapishwa: 23/07/2020