Muulizaji: Nina kitabu cha Shaykh Ahmad an-Najmiy (Rahimahu Allaah) na cha Shaykh Zayd al-Madkhaliy (Rahimahu Allaah), vitabu ni “al-Irhaab” na “al-Mawrid al-´Adhb az-Zulaal”. Humo wanatahadharishwa wanachuoni kama Salmaan al-´Awdah, Naaswir al-´Umar, ´Aaidh al-Qarniy, Yuusuf al-Qaradhwaawiy na Muhammad al-´Ariyfiy. Nimevisoma vitabu hivi na kuona kuwa vimesifiwa na Shaykh Swaalih al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah). Nimeshangazwa sana…

al-Luhaydaan: Kwa nini umeshangazwa?

Swali: Je, ni sahihi kuwa Shaykh Swaalih al-Fawzaan na Shaykh Ahmad an-Najmiy wanatahadharisha juu ya Salmaan al-´Awdah na wengineo?

al-Luhaydaan: Hivyo ndivyo ulivyosoma?

Muulizaji: Ndio, hivyo ndivyo nilivyosoma. Ni matahadharisho kwao.

al-Luhaydaan: Wako katika haki – Allaah akitaka.

Muulizaji: Ni sahihi kutahadharisha juu yao?

al-Luhaydaan: Hii ina maana kwamba usiwapupie.

  • Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Muhammad al-Luhaydaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=157277
  • Imechapishwa: 23/07/2020