al-Albaaniy: Anastahiki kuelezwa kwa sifa hiyo (yaani kuwa ni mpotevu), ikiwa anamaanisha al-Ghazaaliy wa sasa. Ni sahihi.

Swali: Vitabu vya al-Ghazaaliy?

Muulizaji: Nido.

al-Albaaniy: Yote mawili. Huwezi. Wengine wanaweza. Mtu mwenye kusoma vitabu vya al-Ghazaaliy anatakiwa kuwa mwanachuoni katika Qur-aan na Sunnah ili asipotee na huyu mpotevu al-Ghazaaliy. Umesikia jibu?

Muulizaji: Ndio.

al-Albaaniy: al-Ghazaaliy ni mtunzi mzuri na anaongea vizuri na anaathiri nyoyo za vijana. Wanapotea na upotevu wake. Ikiwa mtu hana ufahamu sahihi, haiwezekani kwa mtu akaepuka upotevu wake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (591)
  • Imechapishwa: 23/07/2020