al-Waadi´iy kusema Bismillaah katika wudhuu´

Swali: Ni ipi kauli unayoonelea kuwa ina nguvu kuhusu kusema “Bismillaah” kabla ya kutawadha?

Jibu: Tulikuwa tunasema mwenye kutawadha pasi na kutaja jina la Allaah [wudhuu´ wake hausihi] na tulitoa fatwa kwa kauli hii siku zote na kwamba wudhuu´ wake ni batili na hili linapelekea kutosihi kwa Swalah yake.

Hata hivyo ndugu yetu muheshimiwa Shaykh ´Abdul-´Aziyz al-Buraa´iy (Hafidhwahu Allaah) aliandika kijitabu ambacho nilisoma sehemu kidogo au nilikisoma chote na tukaona kuwa dalili zinaonesha kuwa ni bora kufanya hivo [kusema Bismillaah].

Ama Hadiyth ambazo zinaonesha kuwa ni miongoni mwa masharti ya kusihi kwa wudhuu´, ni dhaifu sana. Si sahihi zikatumiwa.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=2959
  • Imechapishwa: 03/05/2015