Swali: Damu inayomtoka mtu puani, kwenye donda au damu ya ugonjwa (istihaadhah) inafanya nguo kuwa najisi na inatengua Wudhuu?

Jibu: Hakuna kinachofanya nguo kuwa najisi isipokuwa damu ya hedhi na nifasi. Ama hizi sio najisi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika ya muumini hanajisiki.”

Vilevile isitoshe Maswahabah walikuwa wanaswali na madonda yao au kwa nguo zao ambazo wakati mwingine zilikuwa zinalowa kwa sababu ya madonda yao. Hivyo sio najisi. Isipokuwa damu ya hedhi na nifasi.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=2258
  • Imechapishwa: 03/05/2015