al-Waadi´iy kuhusu Takbiyr za pamoja siku ya ´iyd II

Swali: Lini inaanza Takbiyr kwenye ´Iyd al-Fitwr na lini inaisha? Na kwenye ´Iyd al-Adhwhaa lini inaanza na lini inaisha?

al-Waadi´iy: Tumekwishajibia hili. Katika ´Iyd al-Fitwr ni wakati watu wanatoka katika swalah na kabla ya swalah, ama baada yake hakuna ubaya wakaleta Takbiyr siku ileile ya ´Iyd. Ama ´Iyd al-Adhwhaa ni katika yale masiku ya kuchinja lakini kusiletwe katika swalah zilizobaki bali kunaletwa Adhkaar za kawaida.

Muulizaji: Je, kila mtu alete Takbiyr kivyake?

al-Waadi´iy: Kila mtu aleta kivyake na inapasa kuwa namna hii, au mmoja akaleta Takbiyr na wengine wakaitikia au wakaleta kikundi. Lakini lililo bora ni kila mtu kuleta kivyake.

Muulizaji: Je, waweke kikomo idadi ya Takbiyr au hapana?

al-Waadi´iy: Takbiyr ni mkusanyiko. Na uchache wake ni Takbiyr tatu na wakizidisha hakuna ubaya.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://muqbil.net/fatwa.php?fatwa_id=64
  • Imechapishwa: 30/07/2020