al-Waadi´iy kuhusu Takbiyr za pamoja siku ya ´iyd

Swali: Ipi hukumu ya kuleta Takbiyr katika ´Iyd al-Fitwr wakati mtu anapotoka katika nyumba yake mpaka anapofika katika uwanja wa kuswalia? Waendelee na Takbiyr mpaka atapokuja imaam? Inajuzu kuleta Takbiyr kwa sauti ya pamoja kwa aliye uwanjani na hali kadhalika katika ´Iyd al-adhwhaa?

Jibu: Maneno ya Allaah (Ta´ala):

وَلِتُكَبِّرُواْ اللّهَ

“Na mumkabiri Allaah.” (02:185)

Hili ni kwa jumla. Wakati wa kutoka kila mmoja ataleta Takbiyr kivyake, na wakileta Takbiyr kwa pamoja naona kuwa haijafikia kiwango cha kuwa ni bid´ah. Lakini haikuthibiti kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahaba wake walikuwa wakileta Takbiyr kwa pamoja. Bora ni kila mmoja alete Takbiyr kivyake. Hali kadhalika wakifika kwenye uwanja wa kuswalia kila mmoja aleta Takbiyr kivyake kwa kuwa haikufanywa wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Na wakileta Takbiyr kwa pamoja nionavyo ni kuwa haijafikia kiwango cha kuwa bid´ah. Kumebaki namna inavyotolewa Takbiyr. Allaahu Akbar Allaahu Akbar, hili… kwa kuwa haikuthibiti namna yake kutoka kwa Mtume (swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutokana na ninavyojua.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://muqbil.net/fatwa.php?fatwa_id=890
  • Imechapishwa: 30/07/2020