Swali: Je, inajuzu kwa mwanamke kusoma Qur-aan ndani ya msahafu na yuko na hedhi?

Jibu: Sijui makatazo yoyote juu ya hili. al-Bukhaariy (Rahimahu Allaah) amepokea katika “as-Swahiyh” yake kutoka kwa Ibn ´Abbaas ya kwamba alikuwa haonelei neno kwa mwanamke mwenye hedhi kusoma Qur-aan. Na hii ndio kauli sahihi katika kauli za wanachuoni. Vilevile Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema kumwambia ´Aaishah:

“Fanya anayofanya mwenye hedhi isipokuwa usitufu Ka´bah.”

mwenye kufanya Hajj husoma Qur-aan pia.

  • Mhusika: Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=758
  • Imechapishwa: 24/09/2020