al-Fawzaan kuhusu mwenye hedhi kuingia msikitini

Swali: Ni ipi hukumu kwa mwenye hedhi kuhudhuria msikitini ili asikilize muhadhara na kukaa sehemu ya nyuma?

Jibu: Haijuzu kwa mwenye hedhi kuingia msikitini na wala haijuzu kukaa humo. Ama kuingia mara moja tu au kukidhi haja yake, hakuna neno. Aingie hata kama atakuwa na hedhi na akidhi haja yake msikitini. Ama kukaa msikitini kwa mwenye hedhi haijuzu, hali kadhalika mwenye janaba mpaka aoge. Asiingie msikitini. Ni haramu kwake hili. Anaweza kusikiliza nyuma ya mlango wa msikiti. Alhamdulillaah kwa leo vipaza sauti vinarusha sauti nje ya msikiti, bali huenda yule ambaye yuko nje ya msikiti akawa anasikia vizuri kuliko yule ambaye yuko ndani ya msikiti.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13267
  • Imechapishwa: 24/09/2020