Swali: Kuna mtu mhabashi anayeitwa ´Abdullaah al-Habashiy anasema kuwa yule anayedai kuwa Allaah Yuko juu ya waja ni kafiri. Anaeneza ´Aqiydah hii kati ya ´Awwaam. Kuongezea juu ya hilo ni kwamba ni Suufiy.

Jibu: Ni mpotevu. Ikiwa ni yule anayeishi Lebanon Shaykh al-Albaaniy amemraddi na wengine katika Ahl-us-Sunnah wamemraddi.

Tunaamini kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Amelingana juu ya ´Arshi:

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

“Mwingi wa huruma amelingana juu ya ´Arshi.” (20:05)

Tunaamini kuwa Yuko juu yetu:

سبحان ربي الأعلى

”Ametakasika Allaah, aliye juu.”

وَهُوَ الْقَاهِرُ فَوْقَ عِبَادِهِ

“Naye ni yu juu ya waja Wake.” (06:61)

إِلَيْهِ يَصْعَدُ الْكَلِمُ الطَّيِّبُ وَالْعَمَلُ الصَّالِحُ يَرْفَعُهُ

“Kwake pekee linapanda neno zuri na kitendo chema hukipa hadhi.” (35:10)

أَأَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يَخْسِفَ بِكُمُ الْأَرْضَ فَإِذَا هِيَ تَمُورُ أَمْ أَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يُرْسِلَ عَلَيْكُمْ حَاصِبًا ۖ فَسَتَعْلَمُونَ كَيْفَ نَذِيرِ

“Je, mnadhani mko [katika] amani na Aliyeko mbinguni [juu] kwamba Hatokudidimizeni ardhini, tahamaki hiyo inatikisika? Au mnadhani mko [katika] amani na Aliyeko mbinguni [juu] kwamba Hatokutumieni kimbunga [cha mawe], basi mtajua vipi [makali] maonyo Yangu.” (67:16-17)

Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipochukuliwa katika safari ya usiku alinyanyuliwa mbinguni. Hakunyanyuliwa kupelekwa baharini, Yemen wala Shaaam. Alinyanyuliwa kupelekewa mbinguni. Mtu huyu ni mpumbavu na ni khabithi. Ninawanasihi msisome kitu chochote kutoka kwake na wala msimsikilize. Ni adui wa Sunnah. Huenda akawa ni kampeni ya maadui wa Uislamu ili awashughulishe Waislamu na batili na uongo wake.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?feature=youtu.be&v=wJYyUPuaf40
  • Imechapishwa: 30/08/2020