al-Madkhaliy kuhusu mtazamo wa Ibn Taymiyyah juu ya kuwachukia Ahl-ul-Bid´ah

Kuhusu yale aliyotaja ndugu yetu – Hamad bin al-´Uthmaan – ya kwamba watu hawa – Ahl-ul-Bid´ah – wanasema kuwa sisi tunatanguliza kuwapiga vita wao kabla hata ya mayahudi na manaswara. Nyinyi tokea lini mnawapiga vita mayahudi na manaswara? Si nyinyi leo mnaosema kuwa manaswara ni ndugu zenu! Mnaonyesha hayo waziwazi kwenye magazeti yenu na mihadhara yenu. Asiyesema hivo anasapoti hilo na analinyamazia. Nyinyi ndio mnawapenda manaswara na mayahudi na kuwapaka mafuta. Ninaapa kwa Allaah ya kwamba sisi ni wenye kujitenga nao mbali kuliko tunavojiweka mbali na Ahl-ul-Bid´ah.

Kuhusiana na maneno ya Shaykh-ul-Islaam bin Taymiyyah (Rahimahu Allaah) ya kwamba inatakiwa kuwapenda Ahl-ul-Bid´ah kwa kiasi na kheri walio nayo na kuwachukia kwa kiasi na shari walio nayo, tumekuta katika maneno ya Salaf kuna wanaosema kinyume na maneno haya ya Shaykh-ul-Islaam (Rahimahu Allaah). al-Baghawiy (Rahimahu Allaah) amepokea ya kwamba Salaf wamekubaliana; kuanzia Maswahabah, Taabi´uun, waliokuja baada ya Taabi´uun na wanachuoni wa Kiislamu, juu ya kuwachukia na kuwasusa Ahl-ul-Bid´ah. Mmesikia vizuri? Maneno haya yanahitaji kuangaliwa vizuri. Haifai kwa Muislamu kushikamana na maneno ya mwanachuoni ili aweze kunusuru batili aliyomo.

Ahl-ul-Ahwaa´ wengi wameshikilia maneno haya ya Shaykh-ul-Islaam na kuyatumia kama silaha dhidi ya yule mwenye kulingania katika Sunnah na kutahadharisha juu ya Bid´ah na kuweka Ahl-ul-Bid´ah katika ngazi wanayoistahiki.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/site/audios/HamadOthman/Divers/05Rabee01.mp3
  • Imechapishwa: 26/08/2020