Tunamshukuru Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) kuona Salafiyyuun wana vijana kama ndugu Hamad ambaye ameyatatua matatizo na utatizi huu kielimu na kwa njia bora kabisa na ya ukamilifu zaidi. Allaah akithirishe mfano wake.

Tunawanasihi vijana Salafiyyuun, na wale ambao walikuwa Salafiyyuun kisha wakaacha mfumo huu, watafute elimu na kusoma vitabu vya Salaf-us-Swaalih na wasidanganyike na vitabu vya waliokuja nyuma ambao hawana elimu juu ya mfumo wa Salaf na hawakusoma Uislamu sahihi na Sunnah. Wanaufafanua Uislamu bila ya elimu na hivyo wakawa wametumbukia katika makosa yanayohusiana na ´Aqiydah, Fiqh, fikira na siasa.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/site/audios/HamadOthman/Divers/05Rabee01.mp3
  • Imechapishwa: 26/08/2020