Muulizaji: Tuna matatizo Yemen. Mkuu mmoja kusini mwa Yemen hivi sasa ameita vita na Jihaad dhidi yao. Wanafunzi wanatakiwa kufanya nini?

al-Luhaydaan: Mnajua kuwa mnatakiwa kuwasapoti watu wa haki dhidi ya watu wa batili kadri na mtakavyoweza.

Muulizaji: Ndio, lakini kuna Shaykh mmoja amedai pamoja na Huuthiyyah ya kwamba ni ndugu zetu. Wameandika mkataba na kadhalika. Baadhi ya watu wameenda kinyume.

al-Luhaydaan: Maafikiano haya ni batili. Mwenye kukadhibisha Qur-aan sio kama yule mwenye kuiamini. Kadhalika mwenye kuwakufurisha Maswahabah tukimtoa ´Aliy, watoto wake wawili na Salmaan. Wanawakufurisha Maswahabah wengine wote kama Abu Bakr, ´Umar na ´Uthmaan. Je, mtu kama huyu ni muumini? Huyu ni ndugu yetu? Si shirki kubwa kumuabudu al-Husayn? Je, mtu kama huyu ni ndugu wa muumini? Haiwezekani. Huyu sio Shaykh bali ni mtu ambaye sio msomi [´Aamiy].

Muulizaji: Wanasema kuwa wanachuoni wameafikiana na yeye. Hivi sasa wanadanganya ya kwamba Shaykh Swaalih al-Fawzaan ameafikiana naye na kadhalika. Wanaeneza haya.

al-Luhaydaan: Wanasema uongo. Hiwezekani. Wanasema uongo. Haiwezekani wanachuoni na waumini wakaafikiana naye.

Muulizaji: Inawezekana tutakunukulia mkataba ili uusikie?

al-Luhaydaan: Hapana, hapana. Huu sio mkataba.

Muulizaji: Ninamaanisha zile pointi walizoandikiana. Humo wameandika ya kwamba ni ndugu zetu, kwamba dini yetu ni moja, kwamba tuache kufanyiana chokochoko na kadhalika.

al-Luhaydaan: Wakati alikuja Raafidhwiy kama huyo kwa ash-Shanqiytwiy akamwambia:

”Sisi tuna dini yetu na nyinyi mna dini yenu.”

Mnajua hili? Mnamjua ash-Shanqiytwiy? Alikuja Raafidhwiy mmoja wa Lebanon na kutaka kujadiliana na yeye. ash-Shanqiytwiy akamuuliza watarejea katika nini. Turejee katika Qur-aan ilihali nyinyi mnaikadhibisha? Huyu mkuu wa ukoo ni masikini. Huenda ni mwenye kupenda mali…

Muulizaji: Sio mkuu wa ukoo. Anajinasibisha na elimu na anazungumza.

al-Luhaydaan: Sio kila mwenye kudai elimu [ni mwanachuoni]. Elimu ni amesema Allaah, Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah.

Muulizaji: Tunaweza kukusomea pointi? Ni pointi tatu.

al-Luhaydaan: Sawa.

Muulizaji: Pointi ya kwanza ni utangulizi na unazungumzia makubaliano ya namna ya kueshi na udugu.

al-Luhaydaan: Hapana, hapana. Ni nani mwenye kusema kuwa kafiri na muumini ni ndugu?

قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الَّذِينَ يَعْلَمُونَ وَالَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ

“Je, wanalingana sawa wale wanaouja na wale wasiojua?” (39:09)

Ni nani mwenye kusema hivo? Endelea.

Muulizaji: 

وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّـهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا

”Na shikamaneni kwa kamba ya Allaah nyote pamoja wala msifarikiane.” (03:103)

al-Luhaydaan: Ni kweli. Ni nani mwenye kushikamana na kamba ya Allaah? Ni wale wenye kumuamini Allaah na Mtume Wake. Ni wale wenye kumtii Allaah na Mtume Wake. Wale wenye kumfuata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake ambao amesema juu yao:

”Wale wenye kufuata yale ninayofuata mimi na Maswahabah zangu.”

Muulizaji: Himdi zote ni Zake Allaah aliyesema:

إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ

”Hakika Waumini ni ndugu.” 49:10

al-Luhaydaan: Bila ya shaka. Je, wao ni waumini? Je, mwenye kusema yale yanayosemwa na Allaah:

أُولَـٰئِكَ مُبَرَّءُونَ

”Hao wameepushwa.” (24:26)

ni kama yule mwenye kusema kuwa si sahihi?

Muulizaji: Allaah Mtukufu Amesema kweli. Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad na ukoo wake safi na awe radhi juu ya Maswahabah zake wazuri kati ya Muhaajiruun na Answaar na wale wenye kuwafuata kwa wema.

al-Luhaydaan: Ni Muhaajiruun na Answaar wepi hao? Hamaanishi Muhaajiruun wote ni wanusuraji. Anamaanisha ´Aliy, watoto wake wawili na Salmaan al-Faarisiy. Wanamaanisha hawa tu. Wengine wote wanawakufurisha baada ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Muulizaji: Sote ni Waislamu. Mola wetu ni mmoja, kitabu chetu ni kimoja, Mtume wetu ni mmoja na adui yetu ni mmoja hata kama tuna tofauti kati ya mambo madogo madogo. Sisi kama Waislamu Uislamu umetukataza kukiuka maisha kati yetu, heshima na mali.

al-Luhaydaan: Haya ni maneno yasiyokuwa na maana. Ni maneno ya kweli, lakini yanawahusu tu waumini. Waasi hawa walikuwa si lolote hapo kabla. Walikuwa wanakaribia kutokuwepo Yemen. Walikuwa hawapewi heshima yoyote ile. Hili lilipatikana pindi waislamu walipokuwa wadhaifu na wakapoteza mambo mengi ya dini yao. Mwanzoni mwa mapinduzi ya Raafidhwah Iran wakawapa fedha na kuwachukua na kuwapeleka Qum ili kuwafunza.

Muulizaji: Mwishoni ´Abdul-Maalik al-Huuthiy na Shaykh Muhammad bin ´Abdillaah al-Imaam wamepiga muhuri. Muhuri na kwamba yeye ndio kiongozi wa Ahl-us-Sunnah.

al-Luhaydaan: Kiongozi ni nani?

Muulizaji: Muhammad al-Imaam.

al-Luhaydaan: Ni uongo. Sio kiongozi.

Muulizaji: Muhammad anawakilisha Ahl-us-Sunnah na yule mwingine anawakilisha Huuthiyyah.

al-Luhaydaan: Ina maana ya kwamba wamekubaliana kuwa wao ni Ahl-us-Sunnah tofauti na wale wengine sio Ah-us-Sunnah wao ni Huuthiyyah. Wamekubali wenyewe wako wana makosa.

Muulizaji: Kutokana na haya, kumekhitimishwa mkataba kati ya Answaarullaah (wasaidizi wa Allaah) akiwakilishwa kama ´Abdul-Maalik al-Huuthiy…

al-Luhaydaan: Nani kasema kuwa watu hawa ni Answaarullaah?

Muulizaji: Wao wenyewe wamejiita hivo.

al-Luhaydaan: Hawa ni kama Hizbullaah Lebanon.

Muulizaji: … na Salafiyyuun katika markaz ya Nuur Ma´bar na markaz zingine zote zilizoko chini yake, zenye kuwakilishwa na Shaykh Muhammad bin ´Abdillaah al-Imaam, kuhusiana na pointi zifuatazo:

1- Maisha ya amani baina ya pande zote mbili pasina magonvi…

al-Luhaydaan: Hapa wamekubali wenyewe kuwa wao ni pande mbili na sio pande moja. Allaah anasema:

إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ

”Hakika Waumini ni ndugu.” 49:10

Wamekubali wenyewe kuwa ni pande mbili na sio pande moja.

Muulizaji: … mapigano na fitina pasina kujali hali na sababu itakavokuwa pamoja na uhuru wa fikira na wa utamaduni kwa wote.

al-Luhaydaan: Tazama! Uhuru wa fikira. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mwenye kubadilisha dini yake muueni.”

Huu ni uhuru wa fikira?

Muulizaji: 2- Pande zote mbili zisitukanane kwa kuchokozana na uadui pasina kujali njia na nafasi…

al-Luhaydaan: Raafidhwah hawaaminiki. Ni wafanya khiyana pasijna kujali mkataba wanaofunga. Wanaona kuwa ni halali kwao kuwafanyia Ahl-us-Sunnah wanayowafanyia.

Muulizaji: 2- Pande zote mbili zisitukanane kwa kuchokozana na uadui pasina kujali njia na nafasi.

al-Luhaydaan: Hili linathibitisha ya kwamba wanakubaliana kuwa ni pande mbili na sio waumini wamoja.

Muulizaji: Badala yake kufanyiwe kazi udugu na kushirikiana kati ya kila mtu.

3- Kuendelea na mchakato wa mawasiliano wa moja kwa moja kati ya pande zote mbili ili kukabiliana na aina yoyote ya janga, ajali, tatizo au mwenendo wa mtu au jaribio lolote kutoka kwa upande mwingine ili kuharibu…

al-Luhaydaan: Ni kina nani wenye kupora vijiji na miji?

Muulizaji: Huuthiyyah.

al-Luhaydaan: Je, haya yanaafikiana na mkataba huu?

Muulizaji: Hapana kabisa. Yanaenda kinyume nao.

al-Luhaydaan: Basi mambo ni hivo.

Muulizaji: Wanasema kuwa ametenzwa nguvu na kadhalika.

al-Luhaydaan: Ni nani aliyezisimamisha katika sifa zao? Hapo kabla walikuwa wamekinaika kuwa chini ya Zaydiyyah. Wakati Iran na al-Khumayniy walipoita, al-Khamaa´iniy na mambo yao ya dini machafu yakaja ndio wakaanza kuzungumza hivo. Mtakeni Allaah msaada kwa hali yoyote ile.

Muulizaji: Vipi msimamo wetu kutokamana na hili?

al-Luhaydaan: Nyinyi mnauliza ni yupi mnayetakiwa kumnusuru? Mnataka kuwanusuru wenye makosa dhidi ya watu wa haki?

Muulizaji: Hapana. Ninachomaanisha ni Jihaad na mambo kama hayo yanayoendelea hivi sasa.

al-Luhaydaan: Bila ya shaka.

Muulizaji: Kuna mkuu mmoja mkubwa ameita katika uhamasishaji.

al-Luhaydaan: Anaita kwenye nini?

Muulizaji: Mkuu wa jeshi kusini.

al-Luhaydaan: Anaita katika Jihaad?

Muulizaji: Ndio.

al-Luhaydaan: Mtu huyu amewafikishwa.

Muulizaji: Anasema kuwa atasimama msitari wa mbele uwanjani.

al-Luhaydaan: Mtu huyu amewafikishwa. Lau watu wa kusini wasingelisimama kidete basi wangeliipora Aden, Mukallaa´ na miji mingine yote kusini.

Muulizaji: Hivi wanafunzi wamejigawa kwa Shaykh huyu ambaye amepigia saini mkataba huu.

al-Luhaydaan: Kwani huyu ni mtu wa kwanza anayepotea. Allaah amesema:

وَمَا أَكْثَرُ النَّاسِ وَلَوْ حَرَصْتَ بِمُؤْمِنِينَ

“Na wengi wa watu hawatoamini japokuwa utatilia hima.” (12:103)

Muulizaji: Wanampa udhuru…

al-Luhaydaan: Msimtukane. Tunataraji alifanya Ijtihaad na akateleza. Hata hivyo sio katika wanachuoni mpaka tuseme…

Muulizaji: Kuna wanachuoni waliomraddi. Je, tueneze maneno yao?

al-Luhaydaan: Ndio, yaenezeni.

Muulizaji: Kwa mfano Shaykh Rabiy´ na Shaykh ´Ubayd.

al-Luhaydaan: Hakuna shaka ya kwamba mwenye kuwanusuru Raafidhwah hawa ni mpotevu:

لَّا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ

”Hutokuta watu wanaomuamini Allaah na Siku ya Mwisho kuwa wanawapenda wale wanaopinzana na Allaah na Mtume Wake.” (58:22)

Allaah amesema juu ya mama wa waumini:

أُولَـٰئِكَ مُبَرَّءُونَ

”Hao wameepushwa.” (24:26)

Watu hawa wanasema kuwa ´Aaishah atajitenga kwa al-Mahdiy ili ampige mawe mpaka afe na hali kadhalika Abu Bakr na ´Umar ili awasulubu.

Muulizaji: Shaykh huyu anasema kuwa hatuwapigi vita waislamu wowote mpaka kutumwe Mtume na kutuamrisha kufanya hivyo vinginevyo hapana.

al-Luhaydaan: Haya ni madhehebu ya Raafidhwah. Huwa wanasema kuwa kusipiganywe vita mpaka ajitokeze al-Mahdiy. Walizusha mamlaka ya mwanachuoni ili aweze kucheza mchezo wa al-Mahdiy; al-Mahdiy ambaye bado amejificha pangoni kaskasini mwa Iraq.

Muulizaji: Ninaweza kuwaenezea wanafunzi maneno yako.

al-Luhaydaan: Yaeneze. Huu sio mkataba kabisa. Si jengine zaidi ya shairi la ki-Shaytwaan.

  • Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Muhammad al-Luhaydaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=151324
  • Imechapishwa: 23/07/2020