al-Lajnah ad-Daaimah kuhusu “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy

Swali: Ni ipi hukumu ya Uislamu kwa mwenye kupinga Hadiyth ya uombezi ambayo imepokelewa na al-Bukhaariy katika “as-Swahiyh” yake na anaongeza pia kusema kuwa ndani ya “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy kuna Hadiyth za kuundwa?

Jibu: Hakika “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy imekubaliwa na wanachuoni. Hadiyth zake zinategemewa katika kuthibitisha hukumu na kunasimama hoja kwazo kwa mwenye kwenda kinyume. Mwenye kusema kuwa ndani yake kuna Hadiyth za kuundwa ni mjinga mwenye kukosea ambaye ameenda kinyume na maafikiano ya Ummah. Hali kadhalika mwenye kupinga uombezi mkubwa au Hadiyth juu ya maombezi mengine ambazo zimepokea al-Bukhaariy katika “as-Swahiyh” na maimamu wengine wa Hadiyth ni mwenye kwenda kinyume na Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah na Salaf wa Ummah huu. Anafuata madhehebu ya wapindaji na wapotevu.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (3/345)
  • Imechapishwa: 22/08/2020