al-Hajuuriy aliulizwa katika ”al-Kanz ath-Thamiyn” (04/516):

”Je, njia za Da´wah ni kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah peke yake (Tawqiyfiyyah) au ni kwa Ijtihaad?

Akajibu: Ni kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah peke yake. Kwa kuwa kulingania katika dini ya Allaah ni ´ibaadah. ´Ibaadah ni kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah peke yake.”

Tazama mpendwa msomaji! Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa mujibu wa al-Hajuuriy anaonelea kuwa anakosea katika njia za Da´wah[1] na Mola Wake anamuadabisha na anamrekebisha kosa lake katika njia za Allaah. Kwa hivyo kwa mujibu wake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anaona kuwa anakosea katika jambo ambalo ni la kukomeka (Tawqiyf) na Wahy kutoka kwa Allaah (Ta´ala).

Hapa hatujadili kama Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anafanya Ijtihaad au hapana. Tunachomjadili al-Hajuuriy ni kumtia makosani Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika yale ambayo ni njia za Da´wah na wakati huo huo anasema kuwa njia za Da´wah ni kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah peke yake, kama alivyofutu.

Kusema kuwa anakosea katika ambayo ni Wahy na ya kukomeka ni tendo kubwa la jinai na dhambi ya wazi. Ni mwenye kwenda kinyume na maafikiano ya Ummah yaliyonukuliwa na maimamu wa Uislamu na Salaf na waliokuja nyuma wote waliosema kuwa Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam) wamekingwa na kukosea katika ule Wahy wanaofikisha kutoka kwa Allaah (Ta´ala).

al-Hajuuriy anathibitisha kuwa njia za Da´wah ni kwa kukomeka (Tawqiyf) halafu anamhukumu Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba anakosea katika njia za Da´wah. Tunaomba ulinzi kwa Allaah kutokamana na kukoseshwa nusura. Janga kubwa ni kuona al-Hajuuriy anayatetea maneno haya mabaya kama alivyomraddi az-Zaa´biy katika tovuti yake.

[1] al-Hajuuriy amesema:

”Haya – akimaanisha kisa cha kipofu ´Abdullaah Ibn Umm Maktuum na viongozi makafiri wa Quraysh kilichotajwa katika Suurah ”´Abasa” – ni miongoni mwa njia za Da´wah ambazo alikosea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Mola Wake akamtia adabu na akateremsha Wahy utaosomwa mpaka siku ya Qiyaamah ukirekebisha kosa hili.”

  • Mhusika: Shaykh ´Arafaat bin Hasan bin Ja´far al-Muhammadiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Bayaan al-Fawriy (01/08)
  • Imechapishwa: 11/10/2016