al-Fawzaan vitabu vyake kufanyiwa tarjama katika lugha nyingine

Swali: Ufaransa kuna kampuni ya kuchapisha vitabu ambayo imechapisha baadhi ya vitabu vyako. Hata hivyo hatukuona idhini yako wala jina la mwenye kufasiri. Je, unamruhusu mtu yeyote kufasiri vitabu vyako?

Jibu: Hapana. Hatutoi idhini kwa yeyote. Ni lazima nijue ni nani mwenye kufasiri. Mtaalamu ni lazima apitie ufasiri wake. Watapoikubali ndio nitampa idhini yangu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/adaab-11-08-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 01/05/2015