al-Fawzaan kutumia jino la dhahabu

Swali: Je, inajuzu kutumia jino la dhahabu?

Jibu: Ikiwa anahitajia kuvaa [jino la] dhadhabu kwa dharurah hakuna neno. Ama ikiwa ni kwa ajili ya kujipamba, haijuzu kwa mwanaume kujipamba kwa dhahabu. Ama ikiwa ni kuvaa kwa haja, hakuna neno kufanya hivo kwa sababu dhahabu ina umaalum wake nao ni kwamba haiozi mdomoni. Ama fedha na vitu vinginevyo vinaoza mdomoni na kutoa kutu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/liqo_%20maftuh-20-07-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 03/05/2015