al-Fawzaan kuhusu wazazi wa Mtume na Ibraahiym, Abu Twaalib na mtoto wa Nuuh

Swali: Katika mji wetu Senegal kuna Tijaaniyyah. Wanasema kuwa ni jambo lisilowezekana kwa Abu Twaalib na wazazi wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa Motoni…

Jibu: Makafiri haiwezekani wakawa Motoni? Watakuwa Motoni.

Baba yake na Ibraahiym (´alayhis-Salaam) yuko Motoni. Mtoto wa Nuuh yuko Motoni. Hakutazamwi nasaba na kusema huyu ni mtoto wake na kadhalika. Kinachotazamwa ni imani na kufuata.

Muulizaji: …wanasema vilevile wao ndio wenye kumpenda sana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)…

al-Fawzaan: Haitoshelezi kupenda pamoja na kukosekana kufuata.

الَّذِينَ يَتَّبِعُونَ الرَّسُولَ النَّبِيَّ الْأُمِّيَّ الَّذِي يَجِدُونَهُ مَكْتُوبًا عِندَهُمْ فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنجِيلِ يَأْمُرُهُم بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَاهُمْ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُحِلُّ لَهُمُ الطَّيِّبَاتِ وَيُحَرِّمُ عَلَيْهِمُ الْخَبَائِثَ وَيَضَعُ عَنْهُمْ إِصْرَهُمْ وَالْأَغْلَالَ الَّتِي كَانَتْ عَلَيْهِمْ ۚ فَالَّذِينَ آمَنُوا بِهِ وَعَزَّرُوهُ وَنَصَرُوهُ وَاتَّبَعُوا النُّورَ الَّذِي أُنزِلَ مَعَهُ ۙ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ

“Wale ambao wanamfuata Mtume, Nabii asiyejua kusoma wala kuandika, ambaye wanamkuta ameandikwa kwao katika Tawraat na Injiyl, anawaamrisha mema na anawakataza maovu, na anawahalalishia vilivyo vizuri na anawaharamishia vilivyo vichafu, na anawaondoshea majukumu yao na minyororo ngumu zilizokuwa juu yao. Basi wale waliomwamini na wakamtukuza, na wakamsaidia na wakafuata Nuru ambayo imeteremshwa pamoja naye; hao ndio wenye kufaulu.” (07:157)

Ni lazima kufuata.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/egatht–14340322.mp3
  • Imechapishwa: 19/05/2020