al-Fawzaan kuhusu mtazamo wa Abul-Hasan al-Ma´ribiy juu ya imani

Swali: Kuna kanda sita za Abul-Hasan al-Ma´ribiy ambapo anathibitisha ndani yake kwamba matendo siyo nguzo katika imani, bali ni sharti ya kutimia kwa imani. Ni yepi maoni yako?

Jibu: Hata ikiwa amsema? Sisi hatujali aliyosema Abul-Hasan al-Ma´ribiy wala mwengine yeyote. Waseme watakayo na wasajili watakayo, sisi tunarejea katika Kitabu na Sunnah na mfumo wa Salaf.

Matendo ni katika imani. Imani ni kutamka kwa ulimi, kuamini moyoni na matendo ya viungo. Matendo ni katika imani na si sharti [ya kutimia kwa imani], bali ni katika uhakika wa imani na inaingia ndani ya imani. Matendo ni imani na si sharti ya imani. Kila mmoja huchukuliwa kauli yake na kurudishwa isipokuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kitabu na Sunnah vinafahamisha ya kwamba matendo ni katika imani. Imani ni matawali sabini na kitu, ya juu yake ni kusema: “hapana mungu  wa haki isipokuwa  Allaah” na ya chini yake ni mtu kuondosha maudhi njiani, na hayaa ni tawi katika imani.” Kaifanya imani ni kauli, matendo na kuamini. Kusema “hapana mungu  wa haki isipokuwa  Allaah” ni  kutamka, kuongea kwa ulimi. Kuondosha maudhi njiani ni kitendo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amefanya ni katika imani.

al-Ma´ribiy anasema

“Hapana, hii ni katika sharti ya kutimia kwa imani.”?

Kauli ya nani tuchukue, ya al-Ma´ribiy au ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Na kuw na hayaa ni tawi katika imani. Kuwa na hayaa ni kitendo cha kimoyo. Hatuchukui maoni ya watu hata wakifikia kiwango cha elimu ilioje, ikiwa maoni yao yanaenda kinyume na Qur-aan na Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), sisi tunayaacha na tunachukua alichosema Allaah na Mtume Wake:

فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللّهِ وَالرَّسُولِ

“Na mkizozana katika jambo lolote, basi lirudisheni kwa Allaah na Mtume.” (04:59)

Suala hili limemalizwa na limeandikwa katika vitabu vya ´Aqiydah, ´Aqiydah ya Salaf na ´Aqiydah ya maimamu. Imeandikwa na kufundishwa. Hatuna haja ya maoni ya fulani na fulani.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=123583
  • Imechapishwa: 12/11/2022