Sifa za al-Fawzaan juu ya ”as-Siraaj al-Wahhaaj” cha Abul-Hasan al-Ma´ribiy

Swali: Je, ni kweli kwamba umesifu kitabu ”as-Siraaj al-Wahhaaj fiy Swahiyh-il-Minhaaj” cha Abul-Hasan al-Miswriy?

Jibu: Minhaaj ipi? Mimi ndio mara ya kwanza nakisikia. Ni vipi nikisifu? Naapa kwa Allaah kwamba ndio mara ya kwanza nakisikia. Kitabu ninachokijua ni ”as-Siraaj al-Wahhaaj min Kashf Matwaalib Swahiyh Muslim bin al-Hajjaaj” cha Siwddiyq Hasan Khaaan. Kuhusu kitabu hichi mimi sikijui. Lakini leo ni rahisi kusema uwongo na uzushi. Tusithibtishe maneno yoyote juu yangu mimi wala mwingine yeyote mpaka mwenye nayo alete maandishi, saini au sauti iliyorekodiwa. Pamoja na kwamba sauti pia inaweza kugilizwa, lakini mtu anaweza kupuuzilia jambo hilo. Msiamini uvumi unaoenezwa. Mnaona uwongo leo ni mwingi na kugombanisha kati ya wanazuoni. Tahadharini na jambo hili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tatwhiyr-il-I´tiqaad (8) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/et–1432-04-03.mp3
  • Imechapishwa: 12/11/2022