Swali: Kuna baadhi ya Madu´aat katika chaneli ya satelaiti anasema ya kwamba Ibliys hakumkufuru Allaah. Anasema vilevile kuhusu Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Wanawake ni wapungufu wa akili na dini.”
anasema ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anafanya mzaha nao. Ni yapi maoni yako?
Jibu: Huu ni ukafiri tunamuomba Allaah kinga. Huu ni ukafiri na kukadhibisha Maneno ya Allaah na maneno ya Mtume Wake. Ibliys alivunja amri ya Mola Wake. Kama ilivyokuja katika Qur-aan. “Fasaqah”, yaani alitoka nje ya amri ya Mola Wake. Allaah Akamlaani na kumfukuza na kumuweka mbali. Je, Allaah Humlaani mtu asiyekuwa kafiri? Atamuweka mbali na Rahmah Zake ikiwa sio kafiri? Ikiwa Ibliys sio kafiri, iko wapi kufuru juu ya uso wa ardhi? Tunamuomba Allaah afya. Huyu anamkadhibisha Allaah na Mtume Wake na Ijmaa´ ya Waislamu. Ama kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

Hili limethibiti kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Aliulizwa kuhusu hilo, akasema:
“Upungufu wa akili zao”, ni mahala pa wanawake wawili kushuhudia anashuhudia mwanaume mmoja. Hii ni dalili inayoonesha upungufu wao wa akili na kutokuwa madhubutu katika ushuhuda. Ama “upungufu wa dini yao”, ni kule kupitikiwa na wakati ambapo hawezi kuswali, kama wakati wa hedhi na nifasi. Tofauti na mwanaume ambaye yeye anaswali daima. Upungufu wa dini yao ni katika njia hii.
Hakuna mwenye kumradi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) isipokuwa kafiri. Tunamuomba Allaah afya. Mwanamke ni mpungufu wa akili na dini sawa akipenda hilo au akatae. Allaah ndiye Kamuumba namna hiyo. Allaah ndiye Kamuumba namna hiyo.
وَلَيْسَ الذَّكَرُ كَالْأُنثَىٰ
“Na mwanamme si kama mwanamke.” (03:36)
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13342
- Imechapishwa: 28/07/2020

Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13342
Imechapishwa: 28/07/2020
https://firqatunnajia.com/al-fawzaan-kuhusu-maneno-ya-amr-khaalid/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)